NCCR-Mageuzi zafungua ofisi

HomeKimataifa

NCCR-Mageuzi zafungua ofisi

Baada ya kutokea vurugu zilizosababisha Ofisi za Makao Makuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi zilizopo Ilala mkoani Dar es Salaam kufungwa na kuwekwa chini ya ulinzi mkali wa polisi, sasa zimefunguliwa.

Taarifa za ufunguzi wa Ofisi hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho, Anthony Komu ambaye aliwataka wanachama kutokuwa na wasiwasi na badala yake wafike ofisini kujenga chama kwa kuwa ofisi zipo katika mikono salama.

“Nawaomba wanachama na wananchi wote wenye kuhitaji huduma ya chama chetu waje wasiwe na wasiwasi na hata wale waliosimamishwa uongozi tunawakaribisha waje waeleze nia na madhumuni ya kufanya kile kilichofanyika kwa sababu bado ni wanachama wetu,” alisema Komu.

Kuhusu Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, James Mbatia, Komu alisema kiongozi huyo hakufika jana kutokana na majukumu mengine ya kichama na kuongeza kuwa leo atafika asubuhi na kuendelea na majukumu yake.

error: Content is protected !!