NMB yazindua ATM ya kubadili fedha Uwanja wa KIA

HomeKitaifa

NMB yazindua ATM ya kubadili fedha Uwanja wa KIA

Benki ya NMB jana imezindua mashine ya kutolea fedha (ATM) ya kwanza katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Kilimanjaro (KIA) yenye uwezo wa kubadili fedha za kigeni kwenda shilingi za Kitanzania.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi, Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna alisema wateja na hata wasio wateja wa NMB sasa wanaweza kubadilisha fedha hadi kiasi cha Dola za Kimarekani 2,000 kwa wakati mmoja.

“Kwa kuanzia, mashine hii itakuwa ina uwezo wa kubadili Dola za Marekani, Euro za Umoja wa Ulaya na Paundi ya Uingereza kwenda shilingi ya Tanzania,” alisema Zaipuna.

Uzinduzi wa mashine hiyo (FX ATM) ni hatua nyingine muhimu kwa Benki ya NMB ya utoaji huduma kwa Watanzaia wanaosafiri kutoka nje, watalii na wageni wengine wanaokja nchini Tanzania.

Uwepo wa mashine hiyo umelenga kuboresha huduma za ubadilishaji wa fedha uwanjani hapo ambapo mteja atakuwa na fursa ya kujihudumia mwenyewe kwa saa 24.

error: Content is protected !!