Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa amesema hajaridhiswhwa na gharama za upanuzi wa kituo cha afya Naipanga kilichopo Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi kwa kusema kiasi cha shilingi milioni 600 zilizotumika haziendani na uhalisia wa majengo yaliyojengwa, kufuatia hatua hiyo Mhe Kassimu Majaliwa ameagiza Mganga mkuu wa wilaya ya Nachingwea Dk Charles Mtahbo, asihamishwe au kuondoka katika wilaya hiyo hadi atakapokamilisha ujenzi wa majengo yote pamopja na baraza za kuwatembezea wagonjwa.
Ukaguzi wa mradi huo wa upanuzi wa kituo cha afya ni muendelezo wa ziara ya Waziri mkuu katika ukaguzi wa miradi ya maendeleo mkoani Lindi, Ambapo amesema Serikali imetoa muongozo katika maeneo yote yanayojengwa vituo vya afya kwa kiasi cha shilingi milioni 400 hadi 500 kinakuwa kimekamilika.
> Waziri Mkuu akagua Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi
Katika ziara yake amekagua mradi wa shule ya Sekondari maalum ya wavulana wa masomo ya sayansi Waziri Mkuu ametoa pongezi kwa wananchi wa kijiji cha Chiumbati kwa kujitolea eneo bure kwa serikali ili kuwezesha ujenzi wa shule hiyo.
Mradi huo wa shule unatekelezwa kwa ushirikiano wa michango ya wananchi, fedha kutoka serikali kuu pamoja na mapato ya ndani ya Halmashauri na awamu ya kwanza itagharimu shilingi milioni 556, Mradi huo unatarajia kuwa na Madarasa 32, Nyumba za walimu 20, maabara za kemia, fizikia, bailojia, mabweni 20 utaweza kuwahudumia wanafunzi 1600.