Filamu ya Dune inaanza na amani kana kwamba ni ile “happily ever after” ambayo huonekana katika filamu nyingi. Amani inavurugika baada ya Sayari ya Arrakis kuvamiwa na majeshi ambayo hawana utu wala kuua mamilioni ya watu, wanatekeleza mauwaji ya kinyama kwenye Sayari hiyo.
Majeshi hayo yanawateketeza viumbe jamii ya Fremen ambao ndiyo wakazi wa sayari ya Arrakis. Waarakis wanauliwa wengi na tena kwa mafungu na kufanya majeshi mengine kuungana ili kumkabili adui ambaye teknolojia yake, siyo yake ni kubwa zaidi. Hakuna kitu kinauma kama kuwa mdhaifu kwenye familia, yaani wakati wenzio wote wana nguvu za kupambana na kujilinda, inabidi wafikirie na kukulinda na wewe kwa kuwa hauwezi kujifanyia hivyo.
> ‘My Name’ Filamu itakayonogesha wikiendi yako
Hiyo ndiyo hali anayokutana nayo Paul ambaye amezaliwa ili awe kiongozi lakini ndani yake, anahisi kuwa huo siyo wito wake.
Wakati familia yake ikiwa imezungukwa na walinzi wenye miili iliyojengeka, Paul anaonekana ni goigoi asiyejua hata kushika kisu. Hata hivyo, wahenga walisema, umdhaniaye siye kumbe ndiye.
Usaliti wa kugeuza rafiki adui, safari ya kutafuta mwito halisi wa maisha na nguvu ya huba, ni sehemu ya kinachowasilishwa na wasanii mahiri akiwemo Timothée Chalamet, Rebecca Ferguson, Dave Bautista, Zendaya na Jason Momoa.
Unasubiri nini, katazame filamu ya Dune nisije nikakumalizia uhondo wote.