Ukatili kwa waandishi wa habari wapungua

HomeKitaifa

Ukatili kwa waandishi wa habari wapungua

Ofisa Programu Mwandamizi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Paul Malimbo amesema matukio ya waandishi wa habari kupigwa, kunyang’anywa vifaa vyao vya kazi, kunyimwa taarifa, kukamatwa, kutishwa na kufungiwa kwa vyombo vyao yamepungua ikilinganishwa na miaka miwili iliyopita.

Malimbo aliyasema hayo jana kwenye maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya kukomesha ukatili dhidi ya wanahabari huku akieleza kwamba kwa miezi 10 iliyopita waandishi 23 walikumbwa na mikasa midogo na kuanzia January hadi oktoba mwaka huu vyombo vitatu ya habari vilifungiwa.

“Kipindi hiki kilikuwa na matukio mengi ya magazeti kufungiwa na vituo vya televisheni kutozwa faini,” alisema Malimbo.

error: Content is protected !!