Tanzania inajivunia raia wake wengi waliowahi kuhudumu katika ngazi ya Kimataifa kupitia taasisi mbalimbali.
Miongoni mwa Watanzania hao, kuna wanawake ambao wamewahi au wanaendelea kushika nafasi kubwa kwenye taasisi za Kimataifa.
Hapa chini ni majina ya wanawake watano wa Kitanzania waliowahi kuwa katika nafasi kubwa zaidi Kimataifa;
5. Maryam Salim Ahmed
Mtoto huyo wa Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt Salim Ahmed Salim, kwa sasa ni Meneja wa Benki ya Dunia kwa nchi ya Cambodia.
Amefanya kazi Benki ya Duni kwa zaidi ya miaka 20 sasa ambapo aliwahi pia kuwa Meneja wa taasisi hiyo kubwa duniani kwa nchi ya Albania.
Vyeo vingine alivyowahi kushika ndani ya Benki ya Dunia ni Mshauri katika ofisi ya Mtendaji Mkuu, Makamu wa Rais anayehusika na uendeshaji na Mshauri wa Uendeshaji.
4. Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka
Mwaka 2005, Serikali ya Zimbabwe ilianzisha mpango wa kuwaondoa wafanyabiashara na watu wengine ambao ilisema wameka kiholela katika maeneo mbalimbali. Mpango huo uliitwa ‘Operation Murambatsvina’.
Oparesheni hiyo ilipingwa kwa madai kwamba uliwalenga wapinzani wa Serikali jambo lililomfanya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atume mjumbe wake maalum nchini humo ili afanye utafiti wa kina na kutoa taarifa kuhusu ‘Operation Murambatsvina’.
Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, alikuwa Mtanzania, Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka.
Profesa Tibaijuka pia aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Makazi Duniani (UN-HABITAT) kuanzia mwaka 2002 (kabla ya hapo Shirika hilo lilitambulika kama Kituo cah Makazi Dunia ambapo kilipanda hadhi chini ya uongozi wa Profesa Tibaijuka aliyekiongoza kuanzia mwaka 2000)
3. Dkt Stergomena Tax
Mwanamke wa kwanza kuwa Waziri wa Ulinzi wa Jeshi la Kujenga Taifa wa Tanzani, Dkt Stergomena Tax amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
2. Getrude Mongela
Rais wa Kwanza wa Bunge la Umoja wa Afrika ni Mtanzania Getrude Mongela.
Bi Mongela pia amewahi kuhudumu katika Umoja wa Mataifa akisimamia miradi mbalimbali inayohusu wanawake.
1. Dkt Asha-Rose Migiro
Dkt Asha Rose Migiro ambaye kwa sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, ndiye mwanamke wa Kiafrika aliyewahi kushika nafasi kubwa zaidi kwenye Umoja wa Mataifa.
Alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuanzia mwaka 2007 hadi 2012.