Kwa mujibu wa mtandao maarufu wa TMZ kutoka nchini Marekani, Kanye West bado anaamini kwamba Kim Kardashian ni mkewe kwani mchakato wa talaka yao haujakamilika. Kwa miezi miwili sasa Kanye na Kim wamekuwa wakifuatilia talaka yao ambayo inasemekana mchakato wa kukamilika unakwenda vizuri.
Kwa namna inavyoonekana ni dhahiri kwamba Kanye bado ana mapenzi mazito na Kim licha ya kuwa katika mchakato wa talaka. Hii ni kutokana na Kanye kutumia neno “bado ni mke wangu” kwenye mahojiano yake mbalimbali.
Licha ya kuonekana kupeana ‘support’ kwenye shughuli zao baada ya Kim kuonekana akitoa mchango mkubwa kwenye uzinduzi wa album ya Kanya (Donda), lakini mchakato wao wa talaka haujakoma.
Hivi karibuni Kanye alitangaza kuuza moja ya mjengo wako, katika hali ya kushangaza mjengo huo ulinunuliwa na mkewe Kim Kardashian kwa dola za kimarekani milioni 23. Hatua hiyo inachukuliwa kama ni moja ya dalili kubwa kuwa mchakato talaka yao uko pale pale.