Maria Zayumba anadaiwa kumwiba mtoto wa kike mwenye umri wa miaka sita anaesoma darasa la kwanza Mkoani Morogoro, kisha kumsafirisha na kwenda nae Iringa ili kumridhisha mume wake Maria alitenda tukio hilo Oktoba 22 mwaka huu baada ya kumrubuni mtoto huyo wakati anatoka shule kwa kumwambia anampeleka nyumbani.
Kamanda wa polisi Mkoani Morogoro Fortunatus Musilimu anasema walipolkea taarifa ya kupotea kwa mtoto huyo iliyotolewa na mamaake katika kituo kikuu cha polisi Morogoro, Kesi hiyo ilipewa RB namba MOR/RB/9089/2021 na juhudi za kumpata mtoto huyo awali zilishindikana.
Mtoto huyo alikuja kupatikana baada ya mama mmoja kumuona mtoto huyo wa jirani yake akiwa na mtu ambaye hamfahamu, Mama huyo alimfuata na kumuuliza uhusiano wake na mtoto na alishindwa kujibu ndipo watu walimdhibiti na kutoa taarifa polisi.
Mtoto huyo alirudishwa kwa wazazi wake ili aendelee kupata malezi bora huku Jeshi la Polisi kupitia dawati la jinsia na watoto linaendelea kumhoji mtuhumiwa kuhusiana na tuhuma za wizi wa mtoto na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.