Rais Samia atoa kibali cha ajira kwa watumishi 21,200

HomeKitaifa

Rais Samia atoa kibali cha ajira kwa watumishi 21,200

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia kibali cha kuajiri watumishi 21,200 wa Kada za Ualimu na Afya.

Idadi ya Watumishi watakaoajiriwa katika Kada za Ualimu ni 13,130 ambao watafundisha katika shule za Msingi na Sekondari.

Aidha idadi ya watumishi watakaoajiriwa katika kada za Afya ni 8,070 ambao watafanya kazi katika Hospitali za Halmashauri, Vituo vya Afya na Zahanati.

Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Angellah J. Kairuki, leo Aprili 12, 2023 wakati akizungumzwa na waandishi wa habari.

error: Content is protected !!