Spika Ndugai akemea sharti la kuajiri tu waliopita JKT

HomeKitaifa

Spika Ndugai akemea sharti la kuajiri tu waliopita JKT

Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema sharti la kuajiri tu vijana waliopita Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ni la kibaguzi ambalo halipaswi kuvumiliwa kwa kuwa linawaacha wengi nje pamoja na kigezo cha kupima urefu wa mtu ili apate nafasi ya kujiunga polisi au Jeshi la Wananchi.

“Hilo hata mimi naliona, ni ubagauzi mtupu maana vijana tulio nao kwa sasa ni wengi mno ambao makambi yetu hayawezi kuwachukua wote, lazima tuwe wa kweli katika hilo,” alisema Ndugai.

Kauli hiyo aliitoa jana Bungeni baada ya mbunge wa Viti Maalumu, Ng’wasi Kamani wakati akichangia Mwongozo wa Mpango wa Serikali, kuwa vijana na wanyimwa fursa za ajira wakati uwezo wa makambi ya JKT kuwachukua vijana wote ni mdogo.

Kwa mujibu wa Kamani, hata waliomaliza kidato cha sita, mara nyingine wanachukuliwa kufuatana na alfabeti za majina yao, hivyo wenye majina ya mwanzo ndio hubahatika hata kama ufaulu wao ni mdogo.

error: Content is protected !!