Mamlaka ya magereza nchini Uingereza imempa ruhusu Julian Assange ambaye ni muazilishi wa mtandao WikiLeaks kufunga ndoa na mchumba wake Stella Morris akiwa gerezani. Muda huu Assange yupo mahabusu nchini Uingereza ambapo anasubiri uamuzi wa mahakama kuangalia uwezekano wa yeye kufarishwa na kwenda kusomewa mashitaka yake nchini Marekani.
Assange anatafutwa kwa udi na uvumba na Washington Marekani kufuatia kitendo chake ya kuvujisha nyaraka za siri za serikali ya Marekani.
Mchumba wa Assange Stella Morris aliwahi kuwa mwanasheria wake, na sasa wamebahatika kupata watoto wawili wa kiume Gabriel na Max.
Julian Assange mwenye mwenye umri wa miaka 50 alikamatwa Uingereza mwaka 2019 baada ya kuishi ndani ya ubalozi wa Ecuador nchini Uingereza kwa miaka saba kwa kukwepa kusafirishwa kupelekwa nchini Sweden ambapo alikuwa anakabiliwa na makosa ya unyanyasi wa kingono, licha mashtaka hayo baadae yalitupiliwa mbali baadae baada ya ushahidi kukosekana.
Serikali ya Marekani inamshutumu Assange kwa makosa 18 likiwemo kubwa la mwaka 2010 ambapo alivujisha nyaraka za siri zaidi ya 500,000 ambazo zinalihusu jeshi la Marekani katika harakati zake nchini Afghanistan na Iraq. Kama atakutwa na hatia basi anaweza kufungwa miaka 175.