Jeshi la Polisi kufanya msako nyumba kwa nyumba

HomeKitaifa

Jeshi la Polisi kufanya msako nyumba kwa nyumba

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limewataka wananchi wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kutumia fursa ya mwezi mmoja iliotolewa na serikali kusalimisha kwani baada ya hapo watafanya msako wa nyumba kwa nyumba.

Kamanda wa kanda ya Dar es Salaam Jumanne Muliro alisema baada ya muda uliotolewa na serikali kupita msako wa eneo kwa eneo, nyumba kwa nyumba utafanyika ukiongozwa na taarifa za kiintelejensia lengo likiwa ni kuhakikisha wanaomiliki silaha kinyume cha sheria wanakamatwa na hatua kuchukuliwa.

Awali agiizo la kusalimisha silaha hizo lilitolewa hivi karibuni na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene ambapo tamko la msamaha linaisha Novemba 30 mwaka huu. Pia kamanda Muliro aliwakumbusha wanaosalimisha silaha hizo ndani ya muda uliowekwa wazipeleke katika vituo vyote vya polisi, Ofisi za Serikali za mitaa na kwa watendaji wa kata kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa 10 jioni.

error: Content is protected !!