Ujenzi Bandari ya Bagamoyo unavyochochea vita China na India

HomeKimataifa

Ujenzi Bandari ya Bagamoyo unavyochochea vita China na India

Hivi karibuni kumekuwa na mvutano wa kati ya mataifa mawili makubwa duniani, China na India. China na India kwa miezi 17 mlulizo katika eneo la ladakh, huku kila mmoja ameweka majeshi yake tayari kuanza vita kama aneo la mpaka. Mara kadhaa wanajeshi hao wameripotiwa kufyatuliana risasi na kusababisha vifo na hasara kubwa.

Sasa ni kwa namna gani ujenzi wa mradi wa Bagamoyo unaweza kuchochea vita kati ya China na India?

Kauli ya Rais Samia baada ya kuingia madarakani kuwa, serikali yake inafanyia kazi uwezekano wa kufufua ujenzi wa bandari ya Bagamoyo, inaonekana kuwa kauli mbaya sana kwa Taifa la India.

Kwa miaka mingi sana Serikali ya India imekuwa ikitegemea na kujiimarisha vilivyo kiulinzi na kiusalama katika bahari ya Hindi, ushiriki wa China katika ujenzi wa bandari ya Bagamoyo unahofiwa na India kuwa China inaweza kuitumia Bandari hiyo kwa shughuli za kijeshi dhidi yake. Maeneo ya Magharibi na Kusini mwa Taifa la India hayatokuwa salama kutokana na kuzingirwa na China kupita bahari ya Hindi.

Juni 2021 Rais Samia aliripotiwa kuzungumza na Rais wa China, Xi Jingping, siku chache tu baada ya kutoa kauli kwamba Tanzania inaangalia mpango wa kufufua ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Mwaka 2013 Xi Jinping baada ya kuingia madarakani, ziara yake ya kwanza alifanya Tanzania wakati huo Tanzania ikiwa chini ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Ziara ya Xi Tanzania ilishuhudia kutia saini makubaliano ya awali ya ujenzi wa mradi wa Bagamoyo kati ya kampuni kubwa ya ujenzi wa bandari ya serikali ya China “China Merchants Holdings International” pamoja na Tanzania. Mwendelezo wa makubaliano hayo haukuwa mzuri baada ya Hayati Magufuli kuingia madarakani na kuzuia kabisa mwendelezo wa mchakato ya Bandari ya Bagamoyo.

Baada ya mradi wa Bagamoyo kuingia nyongo, China ikawekeza nguvu na juhudi zake katika ujenzi wa bandari ya Djibouti ambapo China amejenga kambi yake ya kijeshi ya kwanza kabisa nje ya mipaka ya Taifa lake, na kambi hii ni kambi ya kwanza kabisa ya China barani Afrika inayotishia usalama wa mataifa mengi makubwa ikiwemo Marekani.

Serikali ya India imeikuwa ikiimarisha ulinzi wa Taifa lake katika bahari ya Hindi kwa kushirikiana kwa karibu na mataifa ya Mauritius na Sychelles kupitia upande wa Magharibi mwa Taifa la India.

Tanzania na India wamekuwa na uhusiano mzuri tangu wakati wa vita baridi kati ya Urusi na Marekani. Tanzania na India zinafanya biashara 16%, hivyo kulifanya Taifa la India kuwa moja ya mataifa makubwa yanayofanya biashara na Tanzania. Kwa mujibu wa kituo cha uwekezaji cha Tanzania (TIC), uwekezaji wa India nchini Tanzania ni dola bilioni 2.2.

Je, ujenzi wa bandari ya Bagamoyo unaweza kuchagiza zaidi kutokea kwa vita kati ya India na China, je? na hali hii inaweza kuteteresha hali ya kimahusiano baina ya India na Tanzania?

error: Content is protected !!