Tafahadhari: Jifunze namna ya kujilinda na nyoka wakati huu wa joto kali

HomeElimu

Tafahadhari: Jifunze namna ya kujilinda na nyoka wakati huu wa joto kali

Hali ya joto kali haijawahi kuwa rafiki kwa nyoka. Wakati wa joto kali nyoka huangaika kutafuta maeneo yenye kivuli wasipoteze maisha. Upo uwezekano mkubwa wa kukutana na nyoka hasa wakati huu ambao tunapita kipindi cha joto kali hapa nchini Tanzania.

Nyoka hupendelea kuishi maeneo yenye nyasi au majani marefu, au kukaa chini ya mawe au kivuli cha mti. Katika wakati huu inawezekana pia ukamkuta chumbani mwako, ndani ya mkoba au hata kabatini.

Kulingana na mazingira kama hayo, zipo hatua kadhaa za kufuata ili kujilinda na uvamizi wa nyoka hasa wakati huu wa joto kali katika mazingira unayoishi.

1. Epuka kuacha madirisha wazi kwa muda mrefu sana. Cobras na Mambas wanaweza kufikia urefu ambao ni wa juu sana. Nyoka hawa wanaweza kupanda urefu ambao ni ngumu kuwaza kuwa wanaweza, hivyo kwa kuacha madirisha wazi nyakati kama hizi, itakuweka hatarini.

2. Epuka kuacha milango wazi nyakati za mchana au jioni. Ni ngumu kuhisi kuwa nyoka anavamia makazi yako. Kitendo cha kuacha milango wazi kwa kisingizio cha kupata hewa safi kutoka nje, kinaweza kukugharimu.

3. Kabla ya kuketi chini ya miti ili kupata kivuli, ni vyema kutazama hapo unapotaka kusimama pia angalia matawi kwamba hakuna nyoka wanaovizia kwenye matawi hayo.

4. Kung’uta kitanda kabla ya kulala, angalia kitanda chako vizuri na mazingira ya chumba chako kabla ya kulala, nyoka kama cobras wanajulikana kwa kujificha chini ya shuka.

5. Epuka mtindo wa zamani wa kupenda kutulia nje ya nyumba, ukitumia magodoro na kanga jioni. nyoka wengi hupenda kutambaa nyakati za usiku, kutafuta chakula kama panya au wadudu au malazi mazuri.

6. Sio tu nyoka wanaweza kukuuma, lakini pia adui wa zamani wa mwanadamu; centipede (Mosithaphala), ambayo ni ya haraka na yenye sumu kali.

7. Ondoa vichaka katika mazingira ya nyumbani kwako. Vichaka vinavutia panya na wadudu wengine ambao ni vitafunio vinavyopendwa zaidi vya mlo mzuri zaidi wa nyoka.

8. Nunua unga wa kufukuza nyoka na uunyunyize kuzunguka uwanja na pembezoni mwa nyumba yako. Hakika utapunguza uwezekano wa nyoka kutembelea nyumba yako kwa 90%.

Chukua hatadhari, kuna sumu za nyoka ambazo huwezi kudumu hata dakika 10 pindi watakapokuuma, ni muhimu kujilinda.

error: Content is protected !!