Walio wengi wanatamani kuwa na meno meupe yanayong’aa, mara nyingi tunajitahidi kupiga mswaki lakini unakuta bado meno hayang’ai kama vile tunavyotarajia. Wengine huingia gharama kubwa katika kung’arisha meno, lakini zipo njia rahisi za asili ambazo mtu anaweza kutumia kung’arisha meno na zikampa matoke mazuri tu.
zifuatazo ni njia asilia za kung’arisha meno yako
1. Maganda ya ndizi
Inashangaza lakini ina matokeo mazuri kwa mtumiaji. Maganda ya ndizi mbivu yana wingi wa madini ya Magnesium pamoja na pottasium ambayo yana uwezo mkubwa wa kung’arisha meno. Ni rahisi sana kutumia njia hii, baada ya kupiga mswaki, chukua maganda ya ndiz sugua meno yako kwa kutumia upande wa ndani wa maganda hayo, Kisha kusutua vyema na maji ya vuguvugu. Fanya hivyo kwa siku kadhaa, hata kama meno yako yatakuwa na unjano, basi yatasafishika.
2. Mchanganyiko wa baking soda na Hydrogen Peroxide
Baking Soda na Hydrogen Peroxide hutumika katika kazi tofauti kwenye mazingira ya majumbani mwetu, na zote zimekuwa na matokeo mazuri. Lakini vipi kama zitatumika pamoja kwa kuchanganywa kwa minajili ya kusafishia meno? Tiba hii dhidi ya meno yenye unjano inapochanganywa, hutengeneza kemikali ambayo ni nzuri sana kwenye kutakatisha meno, lakini si vyema sana kuitumia mara kwa mara kama ilivyo kwa maganda ya ndizi, kwani inaweza kukusababishia matatizo ya kifya. Ni vyema ukatumia mara moja tu kwa mwaka.
3.Baking soda na mafuta ya nazi
Kwa miaka mingi sana mafuta ya nazi yamekuwa msaada mkubwa sana kwa shughuli mbalimbali za binadamu. Mafuta ya nazi zina utajiri wa virutubisho ambavyo huchagiza ung’arishaji wa meno, hivyo kama yatachanganywa na baking soda, kisha kuingiwa mdomoni na mchanganyiko huo kukaa mdomoni kwa dakika 2-3, kutema na kusukutua kwa maji yenye uvuguvugu, bali bila kukawia utayaona matokeo ya haraka.
4. Baking soda na maji ya limao
Chukua kipande cha limao na kijiko kimoja cha chakula cha baking soda, tumia pamba za masikio kupaka mchanganyiko huu kwenye meno yako na uache kwa muda usiozidi dakika 2 na usiopungua dakika 1. Baada ya hapo, piga mswaki kwa kutumia dawa unayotumia kila siku kuondoa mchanganyiko huo kwenye meno yako
5. Matumizi ya foil na dawa ya meno
Foil au Karatasi ya Aluminium inatakiwa ikatwe katika umbo la mstatili na kisha tumia moja kati ya dawa asilia zilizotajwa hapo juu au unaweza kutumia dawa ya meno unayotumia kila siku. Moja ya tiba twaja hapo juu au dawa ya meno, pakaa vizuri kwenye foil yako uliyoikata kwa umbo mstaili, kisha baada ya hapo vika kwenye meno yako vipande vya foil vyenye dawa kwa dakika kadhaa halafu ondoa usikutue.
unapotumia tiba za nyumbani kumbuka kuzitumia mara kwa mara, kwa sababu hiyo ndiyo njia pekee unayoweza kupata matokeo unayotaka.