Hakuna kitu kinaumiza sana moyo kama kuachwa na mtu ambaye bado unampenda, huu ni wakati ambao mtu unaweza ukahisi maumivu moyoni ukashindwa kufanya mambo yako ya msingi kutokana na mawazo. Wengine hudiriki hata kunywa sumu ili wapotee kwenye uso wa duani au kuanza ulevi na matumizi ya madawa ya kulevya na bangi wakiamini itawapunguzia maumivu na mawazo.
Lakini kitu kimoja cha kuweka akili ni kwamba hakuna mwanzo usio na mwisho, hivyo basi kama umeachwa jua utapata mwanzo mwingine hivyo basi mambo haya 5 unapaswa kujifunza baada ya kuachwa ili uweze kuendelea na maisha kama kawaida.
1. Usilazimishe kupendwa
Mtu anapoachwa huwa anapitia wakati wa huzuni na mawazo hivyo unaweza kujikuta hata kutamani kurudi kwa yule mwenza au mpenzi mbaya na mnyanyasaji kwa sababu unahisi unashindwa kukabiliana na maumivu. Epuka kufanya hivyo na wala usianze kulazimisha watu wakupende kwani unaweza ukaumizwa mara mbili zaidi, wakati wako ukifika utampata wa kwako.
2. Huwezi kumbadilisha mtu
Matukio mengi yamewafanya watu kuwa jinsi walivyo na inabidi uwakubali kama walivyo na kuheshimu maamuzi yao. Kujaribu kuzibadilisha ni zoezi lisilofaa, hivyo kama amekuacha kuna kitu ameona hivyo usilazimishe kujaribu kubadilisha maamuzi yake.
3. Sikiliza walimwengu, epuka kurudia makosa
Ni mjinga tu ambaye hajifunzi kutokana na makosa yake. Rekebisha dosari yako na urekebishe makosa katika kufanya maamuzi. Sikiliza watu wanasema nini kuhusu jambo fulani, kama wewe ni mtu wakuchagua mwenza wa aina fulani na baadaekusihia kuumizwa basi sasa ni wakati wako wkaubadilika.
4. Usikubali fikra mbaya zikutawale
Kama umetoka kwenye mahusiano ya manyanyaso na mtu huyo hakuwahi kukuomba msamaha wala kukiri kosa basi huhitaji msamaha wake na usikubali fikra zikutawale akili mwako kuhusu yeye kwanini hakukuomba msamaha.
5. Kubali kwamba hakuna jambo linalodumu milele
Tunza nyakati nzuri, kubali mbaya lakini kumbuka kuwa hakuna kinachodumu milele. Na hiyo ni sawa.