Amuua mkewe kwa kumlima na jembe kichwani

HomeKitaifa

Amuua mkewe kwa kumlima na jembe kichwani

Mtu mmoja anayefahamika kwa jina la God Sawe anatafutwa kwa kosa la kumuua mke wake Ester juzi saa 12.30 jioni kwa kumlima na jembe kichwa kisha kukimbilia kusikojulikana kwa kutumia usafiri wa bodaboda.

Diwani wa Kibamba, Peter Kilango alisimulia kuwa mtuhumiwa huyo ambaye ni Mchaga wa Machame anajishughulisha na kazi ya kutengeneza friji ambapo siku ya tukio mtuhumiwa alitoka nyumbani na kumuacha mkewe akikanda unga wa ngano kwa ajili ya kuchoma maandazi.

“Mke wake ni mjasiriamali anafanya kazi ya kuchoma maandani na vitumbua na wakati anatengeneza vitu vyake kwa ajili ya kuchoma maandazi na vitumbua, alitoka na kwenda kununua mkaa,” alisema Kilango.

Aliongeza kuwa baada ya Ester kurudi alikuta mlango umefungwa na kushangaa kuwa nani amefunga, mwanamke huyo aliwauliza majirani na kujibiwa kuwa mume wake ambapo alivyogundua ni mume wake aliamua kwenda kwa mjumbe kwa kuwa hawakuwa na uhusiano mzuri na mumewe.

Alieleza kuwa baada ya mjumbe kuelezwa, alikuja na kugonga mlango na mtuhimwa akafungua na kumuamuru mkewe aingine ndani lakini mkewe akakataa kuingia. Aliongeza kuwa kwa kuwa majirani wanafahamu ugomvi wao waliondoka wakiamini kuwa wataelewana tu.

“Wakati wakiwa nje ya nyumba yao mtuhumiwa akamwita mtoto wao anaitwa Ben anasoma darasa la saba Kibamba, lakini mke akamjibu kuwa Ben hayupo nimemtuma dukani. Jibu hilo lilimkasirisha yule bwana wakati amsehikilia jembe anajifanya analima ghafla akamkimbiza mkewe na kumpiga na jembe kichwani,” aliongeza Kilango.

Baada ya mkewe kuanguka chini mtuhumiwa alianza kumponda kichwa mithili ya kulima hali iliyosababisha kupasua kichwa na kukiharibu kabisa. Wananchi waliposhtuka na kujaribu kumkata alikimbia na kufika barabarani na kupanda bodaboda na kutokomea kusikojulikana.

Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Mulito ili kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo, alikiri kutokea kwake na kuongeza taarifa kamili ya tukio hilo ataitoa leo.

 

SOURCES: HABARI LEO

error: Content is protected !!