Maeneo 7 ambayo yalichunguzwa kubaini chanzo cha moto Soko la Karume

HomeKitaifa

Maeneo 7 ambayo yalichunguzwa kubaini chanzo cha moto Soko la Karume

Tume ya uchunguzi wa ajali ya moto uliotokea na kuteketeza Soko la Mchikichini maarufu Soko la Karume, Dar es Salaam jana iliwasilisha taarifa yake kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Makoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla.

Katika taarifa ya kamati hiyo imeonesha kwamba chanzo cha moto huo uliowaacha mamia ya wananchi bila kazi ni mshumaa uliokuwa umewashwa na mraibu wa dawa za kulevya aliyekuwa akiutumia kumulika katika moja ya banda la viatu, ndipo usingizi ukampitia na mshumaa kuteketeza banda hilo na kusambaa.

Katika uchunguzi wake, kamati iliangalia maeneo saba ili kujua pasi na shaka kuwa kipi kilikuwa chanzo cha moto huo.

“Wakati wa uchunguzi tulichunguza vyanzo vifuatavyo kwa kushirikiana na wanakamati wa tume na uongozi wa soko, ambapo tuliangalia kipengele cha makusudi, msuguano wa nyanya za umeme, hitilafu ya umeme au ya kiufundi, moto kuwaka wenyewe, jivu la moto. Vyanzo vyote hivi havikutoa majibu isipokuwa chanzo cha uzembe, uliosababishwa na teja aliyekuwa akitumia mshumaa kumulikia katika moja ya banda la viatu vya fundi viatu na kupitiwa na usingizi na mshumaa kuteketeza banda hilo na kusambaa katika mabanda mengine,” amesema Lukaza.

Mwenyekiti huyo wa tume alisema pia, kijana huyo tayari ameshakamatwa na anaendelea kuhojiwa na Polisi na wenzake watano walikimbia.

Aidha, Makalla ametoa taarifa kwamba Rais Samia Suluhu Hassan ametoa tamko kuwa wafanyabiashara waruhusiwe kuendelea na shughuli zao katika soko hilo kama kawaida.

“Rais Samia Suluhu Hassan amenituma nije nitoe tamko la serikali, amesema anawapenda sana na kwa kuwa anawapenda hakuna sababu ya kusubiri miezi 36 ya ujenzi wa soko, na badala yake mjenge soko wenyewe ili maisha yaendelee,” amesema Makalla.

error: Content is protected !!