Maombi ya Rais Samia kwa viongozi wa dini nchini

HomeKitaifa

Maombi ya Rais Samia kwa viongozi wa dini nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameeleza kukerwa na mauaji yanayoendelea nchini na kusema serikali inalaani matendo yote ya ukatili na mauaji hayo na iko tayari kutafuta suluhu ikibidi kubadilisha sheria au kutunga mpya.

Pia amewaomba viongozi wote wa dini na wananchi kila mmoja kurudisha imani kwa Mungu, ili wamjue na warudi kwenye mafundisho ya dini kwa sababu hakuna dini wala mila inayosema watu wauane.

“Askofu Niweguzi umezungumza suala zima la mmomonyoko wa maadili, ni kweli watu wako mbali na imani za dini zao, niwaombe sana turudi kwenye imani zetu, nitoe wito kwa viongozi wa dini turudi kwenye imani zetu watu wafuate misingi ya imani, sisi serikali tumeona tutaanza kuwafundisha watoto wetu shuleni maadili kwenye somo la uraia,”

“Tunakemea na kulaani matendo yote ya ukatilii na mauaji, na sisi serikali tutatafuta suluhu ikidibi kubadili sheria ambazo tunaona zinahitaji kurekebishwa au tutunge mpya kuhakikisha tunadhibiti vitendo vya ukatili na mauaji,” alisema Rais Samia.

Kauli hizo amezitoa jana wilayani Ngara, mkoani Kagera alipohudhuria sherehe za Jubilei ya miaka 25 ya uaskofu wa Askofu wa jimbo la Katoliki la Rulenge-Ngara, Severine Niwemugizi.

error: Content is protected !!