Diamond, Harmonize kukinukisha Machi 4

HomeBurudani

Diamond, Harmonize kukinukisha Machi 4

Mahasimu wawili kwenye muziki wa bongo fleva nchini Tanzania Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Rajabu Abdul ‘Harmonize’ wanatarajia kuonyeshana mabavu Machi 4, mwaka huu baada ya kila mmoja wao kutangaza kuachia kazi yake siku hiyo.

Wa kwanza kutangaza ni Diamond ambaye alisema Machi 4, mwaka huu ataachia EP yake ya kwanza na kutaka mashabiki zake waweze kuhisi jina la EP hiyo lakini muda mfupi baadaye, Harmonize naye akatangaza kwenye ukurasa wake wa Instagram taarifa kwamba tarehe hiyo ataachia wimbo na kusema kuwa itakua ngoma kali ya mwaka.

“Nimerekodi wimbo wa mwaka, nitauachia 4/3/2022 siku moja kabla ya tamasha kubwa la East African Carnival na nahitaji kila mmoja aje kuimba na mimi maalumu kabisa Bakhresa,’ aliandika Harmonize.

Mashabiki wa wasanii hao watasubiri kwa hamu kazi zao kwani inafahamika kwamba zamani Harmonize ambaye hivi karibuni amejitambulisha kama Bakhresa alikua chini ya lebo ya Wasafi inayomilikiwa na Diamond lakini baadaye kuondoka na kuanzisha ya kwake maarufu kama Konde Gang.

error: Content is protected !!