Mohammed Aboutrika aishukia vikali FIFA juu ya mgogoro wa Ukraine

HomeMichezo

Mohammed Aboutrika aishukia vikali FIFA juu ya mgogoro wa Ukraine

Mkongwe wa timu ya taifa ya Misri Mohamed Aboutrika amelishukia vikali Shirika la Mpira wa Miguu duniani (FIFA) kwa kuitoa nchi ya Urusi kushiriki katika mashindano yote kutoka na uvamizi wake kwa Taifa la Ukraine.

Uamuzi huo ulitoka baada ya Shirikisho la Mpira Ulaya (UEFA) na Pamoja na mataifa kama Uingereza, Poland na mengine kuomba kutolewa kwa Urusi kwenye mashindano yote.

Mohammed Aboutrika anaamini kwamba baraza la mpira wa miguu duniani na mataifa mengine yanapaswa kuchukua hatua kama hizo au Zaidi ya hizo kwenye kukomesha uonevu na dhulumu kwa watu wa Palestina wanofanyiwa na serikali ya Israeli.

“Uamuzi wa kuifungia Urusi lazima uende sambamba na uamuzi wa kuifungia pia Israeli katika mapambano yote kutoka mauwaji ya Watoto na kina mama nchi hiyo inayofanya kwa miaka mingi sana,” alisema Aboutrika.

error: Content is protected !!