Tanzania kutangazwa bure Burj Khalifa mwezi mzima

HomeKitaifa

Tanzania kutangazwa bure Burj Khalifa mwezi mzima

Baada ya kuwa na sitofahamu kuhusu bendera ya Tanzania pamoja na picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kuonekana kwenye gorofa refu zaidi dunia Burj Khalifa kwa siku mbili mfululizo, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amewatoa hofu watanzania kwa kusema kuwa hawajalipa fedha yoyote bali imetolewa kama zawadi na pongezi kwa Rais kutokana na kazi yake nzuri.

“niwaambie wale wanaouliza mmelipa shilingi ngapi, huu ni mwezi wa malkia Burj Khalifa wametoa zawadi kwa mama kwahiyo ile ni zawadi kwa mama ni mwezi wa malkia huu na hatujalipa hata shilingi na taifa hili litatangazwa mwezi mzima huu kupitia Burj Khalifa,” alisema Waziri Kijaji.

Amezungumza hayo alipokuwa akifanya mahojiano katika kipindi cha Power Breakfast cha Clouds na kusisitiza kwamba katika kujenga taifa lazima watu wote washiriki na kwenye kukosoana itumike namna nzuri yakufanya hivyo na sio vinginevyo.

Aidha, Waziri Kijaji alimalizia kwakusema sasa Tanzania ipo tayari kufanya kazi zaidi na kusisitiza watanzania kuingia kwenye uwekezaji na kuchangamkia fursa zilizopo na zijazo.

 

 

error: Content is protected !!