Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amesema kuwa hatua za awali zakuhakikisha wanafunzi wakitanzania waishio nchini Ukraine zimeanza kuchukuliwa na sasa serikali ya Ukraine itawatoa na Urusi itahakikisha wanapita mpakani salama wakielekea Moscow.
“Ukraine itasaidia wavuke lakini wakivuka serikali ya Urusi imetuhakikishia kwamba itaweza kusaidia kuhakikisha kwamba wanafika Moscow,” amesema Waziri Mulamula.
Waziri Mulamula ameeleza kwamba tayari wanafunzi hao wameshapata ruksa yakuvuka mpakani kwani hali ipo shwari kwahiyo wataweza kupita na kufika Moscow salama.
Aidha, amezishukuru serikali za Hungary, Poland na watanzania waishio nchi hizo kwa kuweza kuwasaidia wanafunzi hao kwa kuwapa makazi na huduma umuhimu kipindi hiki cha machafuko nchini Ukraine na Urusi.