Aahidi kufunga taa na kamera Uwanja wa Ndege hadi Posta

HomeKitaifa

Aahidi kufunga taa na kamera Uwanja wa Ndege hadi Posta

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla amesema Serikali ya Mkoa wake inakusudia kufunga taa na kamera za barabarani kuanzia Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere hadi Kariakoo na Posta ili kusaidia kuongeza ulinzi na hasa kulinda miundombinu dhidi ya raia wanaoiharibu wakitafuta vyuma chakavu.

Akiongea wakati wa zoezi la usafi katika Wilaya ya Temeke, amewataka wananchi kuacha kuharibu miundombinu inayowekwa mkoani hapo ili kupendezesha jiji la Dar es Salaam ambalo kwa sasa ni la sita kwa usafi barani Afrika.

Zoezi hilo limeratibiwa na Kampuni ya Sigara nchini (TCC) kwa kushirikisha wadau mbalimbali. TCC ilimkabidhi Mkuu wa Mkoa vifaa vya usafi na kuahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kusafisha na kupendezesha Mkoa wa Dar es Salaam.

error: Content is protected !!