Karani wa Sensa ajinyonga Tabora

HomeKimataifa

Karani wa Sensa ajinyonga Tabora

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Batilda Buriani ametoa taarifa ya kifo cha mmoja kati ya makarani wa Sensa wilayani Igunga mkoani Tabora aliyefahamika kwa jina la Edmund Zakayo ambaye amejinyonga.

Edmund ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Buchenjegele amejinyonga usiku wa kuamkia siku ya sensa huku akiacha ujumbe wa kwamba asilaumiwe mtu yeyote kutokana na tukio la kujinyonga kwake bali ni mgogoro unaohusisha familia yake.

Baada ya tukio hilo, vifaa vyote vya zoezi la sensa alivyokuwa amekabidhiwa marehemu alipewa karani mwingine ambaye alianza kazi yake mara moja.

error: Content is protected !!