Afariki akiigiza filamu ya Yesu

HomeKimataifa

Afariki akiigiza filamu ya Yesu

Mwanafunzi wa Chuo cha Seminari cha Clariantian University nchini Nigeria, Suel Ambrose amedondoka na kufariki akiwa anaigiza filamu ya Yesu maarufu kama “Passion of Christ” siku ya Ijumaa Kuu huku watu waliokuwa wakitazama wakidhani ni utani wa sehemu ya onyesho hilo.

Mavis, mmoja wa wanafunzi anaelezea tukio hilo lilivyotokea na kusema Suel aliyekuwa akiigiza kama Peter alidondoka na kuanza kutokwa na damu puani.

“Alikuwa akicheza uhusika wa Peter kutoka kwenye biblia ile sehemu ambayo anamkata mwanajeshi sikio na Yesu anamponya na kumwambia Peter awaache wanajeshi hao wafanye wanachotaka,

“Baada ya wanajeshi kuanza kuwachukua wanafunzi wa Yesu ndio alidondoka sakafuni na kuanza kutokwa na damu, tulimpeleka kwenye hospitali ya chuo madaktari walifanya juhudi zao lakini hakupata nafuu na ndio tukamuamisha kwenye Hospitali nyingine ya jeshi huko ndipo alipopoteza maisha,” alisema Mavis.

 

 

 

 

error: Content is protected !!