Aliyemchinja mtoto auawa

HomeKitaifa

Aliyemchinja mtoto auawa

Mzee mmoja mkazi wa Siha, Kilimanjaro amepigwa hadi kufa na wananchi wenye hasira kali baada ya kubainika kumchinjwa mtoto wa miaka miwili kijiji cha Ngumbaro kwa imani za kishirikina.

Katika tukio hilo lililotokea Aprili 18 mchana, ndugu wa mtoto Ivani Colomani (2) amesema alianza kumtafuta mtoto huyo baada ya kutoonekana alipokuwa akicheza na wenzie watatu.

Baada ya muda aliona kiatu cha mtoto huyo nje ya mlango wa jirani yao, Jumanne Athumani (63) huku damu zikichuruzika kutokea ndani.

“Baada ya kuona vile nilisogea karibu na kuanza kusukuma kwa nguvu mlango ulipofunguka niliona damu zimetapakaa hapo ndani na kupiga kelele za kuomba msaada, tulikuta huyo mzee akiwa na panga mkononi alikuwa amemchinja mtoto na kumuweka kwenye kiroba”.

Mwenyekiti wa kijiji hicho amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema miili yote miwili imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Kibongoto.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa pia amethibitisha kutokea kwa matukio hayo.

error: Content is protected !!