Agizo la TAMISEMI wanaoomba rushwa upandishaji madaraja walimu

HomeKitaifa

Agizo la TAMISEMI wanaoomba rushwa upandishaji madaraja walimu

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), imebaini uwepo wa vitendo vya rushwa katika upandishaji wa madaraja ya walimu na kuagiza Tume ya Walimu Tanzania (TSC) kudhibiti suala hilo.

Pia, imeagiza kufanyika kwa tathmini na kuona ni idadi gani ya walimu ambao wanastahili kupandishwa madaraja ili suala hilo lifanyiwe kazi kwa haraka.

Naibu Katibu Mkuu wa ofisi hiyo, anayeshughulikia elimu, Gerald Mweli ametoa maagizo hayo alipokuwa akifungua mafunzo kwa walimu jijini Dodoma Septemba 20 mwaka huu.

“Nisingependa kuona hizi shilingi 50,000 zinatumika kuwadai walimu ili majina yao yapelekwe katika upandishwaji madaraja, ninachohitaji kuona ni haki inatendeka,” ameagiza.

error: Content is protected !!