Leo katika historia: Hitler na Churchill waingia kwenye mgogoro

HomeElimu

Leo katika historia: Hitler na Churchill waingia kwenye mgogoro

1. Tarehe kama ya leo mwaka 1934 kimbunga kikali kilikumba Kisiwa cha Honshu, nchini Japan na kuua zaidi ya watu 4,000. Japan inaongoza kwa kukumbwa na majanga ya asili ambayo yamekuwa yakiua maelfu ya watu.

2. Septemba 21, 1909, alizaliwa Dakta Osagyefo Kwame Nkrumah, mwanasiasa na shujaa wa uhuru wa Ghana. Nkurumah alishiriki kikamilifu katika harakati za kupigania uhuru za wananchi wa Ghana dhidi ya mkoloni Mwingereza. Baada ya kujipatia uhuru, kulijitokeza na kushuhudiwa njama kadhaa za kutaka kumwondoa madarakani na hata kumuua Nkrumah.
Mwaka 1966 wakati Dakta Nkrumah akiwa safarini nchini China, Jenerali Joseph Ankrah alifanya mapinduzi na kuiondoa madarakani serikali Nkrumah. Mwanamapinduzi huyo aliaga dunia mwaka 1972 akiwa uhamishoni nchini Romania.

3. Tarehe kama ya leo mwaka 1938 Waziri Mkuu wa Uingereza (wakati huo), Winston Churchill alimshutumu kiongozi wa Ujerumani, Adolf Hitler kwa kuivamia nchi ya Czechoslovakia. Nchi hiyo iligawanyika mwaka 1991 na kuwa nchi mbili za Czech na Slovakia.

4. Mwaka 1949 viongozi wa chama cha kikomunisti cha China walianzisha rasmi Jamhuri ya Watu wa China. Chama hicho kilichoongozwa na mwenyekiti Mao Zedong, kilipigana na kufanya mapinduzi.

error: Content is protected !!