Ahueni kushuka kwa bei ya petroli na mafuta ya taa

HomeKitaifa

Ahueni kushuka kwa bei ya petroli na mafuta ya taa

Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji nchini (EWURA), imetangaza kushuka kwa bei ya petroli na mafuta ya taa huku bei ya dizeli ikiongezeka kwa sh 13 kwa lita.

Mkurugenzi mkuu wa EWURA, Godfrey Chibulunje amesema punguo hilo la bei katika mafuta linachangiwa na kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia.

“Bei za rejareja mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa yaliopelekwa katika bandari ya Dar es Salaam zimepungua kwa shilingi  21 kwa lita moja ya petroli, shilingi 44 kwa mafuta ya taa huku bei ya dizeli ikiongezeka kwa shilingi 13 kwa lita” alisema Chibulunje.

Sambamba na hilo Chibulunje alisema bei za rejareja za mafuta ya petroli na dizeli kwa mkoa wa Tanga, Arusha, Kilimanjaro na Manyara zimepungua kwa shilingi 123 kwa petroli na shilingi 92 kwa bei ya dizeli.

Katika mikoa ya kusini kama Mtwara, Lindi na Ruvuma bei itaendelea kuwa ile ile ambayo ilitangaza Januari kutokana na kutokuwepo kwa shehena ya mafuta iliopokelewa katika bandari ya Mtwara.

Kutokana na tishio la kupanda zaidi kwa bei za mafuta ifikapo Machi na AprilI mwaka huu, Mkurugenzi huyo alisema wanafatilia mwenendo wa bei za mafuta katika soko la dunia ili kuona jinsi gani wanaweza kushauri serikali hatua za kuchukua katika harakati za kupunguza makali ya bei za mafuta.

error: Content is protected !!