Ajira 10,000 za zalishwa katika Mradi wa EACOP

HomeKimataifa

Ajira 10,000 za zalishwa katika Mradi wa EACOP

Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembe, amesema mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Uganda hadi Tanzania umezalisha zaidi ya ajira 10,000 pamoja na kuwajengea wananchi ujuzi mbalimbali wa kiufundi.

Ndejembe ameyasema hayo jana Januari 5, 2026 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari, akieleza kuwa mradi huo ulianza mwaka 2016 na unatarajiwa kukamilika Julai mwaka huu, baada ya kudumu kwa takribani miaka 10.
Amesema kupitia mradi huo, vituo vinne vikubwa vya mafuta kati ya sita vitajengwa nchini Tanzania, hatua itakayosaidia kukuza uchumi wa taifa na kuwanufaisha wananchi wa maeneo yanayopitiwa na bomba hilo.

Kwa upande wake, Waziri wa Nishati na Madini wa Uganda, Ruth Nankabirwa, amesema mradi wa EACOP umegharimu takribani Dola bilioni 4, na umechangia kutoa fursa za ajira kwa vijana pamoja na kuinua uchumi wa nchi husika.

error: Content is protected !!