Akamatwa akiwa amemeza kete 101 za dawa za kulevya

HomeKitaifa

Akamatwa akiwa amemeza kete 101 za dawa za kulevya

Jeshi la Polisi visiwani  Zanzibra linamshikilia Rashid Habib Muhsin (53) baada ya kumkamata akiwa amemeza kete 101 dawa za kulevya aina ya ‘heroin’.

Kaimu Kamishna wa Jeshi la Polisi kitengo cha Dawa za Kulevya Zanzibar, Omar Khamis, alithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo wiki iliyopita baada ya kutiliwa shaka akiwa Uwanja wa Ndege wa Amani Karume akisubiri ndege ya kuelekea Dubai.

Kaimu Kamishna Omar Khamis, amesema mtuhumiwa huyo alikuwa katika hatua za mwisho kuweza kupanda ndege na kuelekea Dubai ndipo alipotiliwa mashaka na kukamatwa.

Rashid Habib Muhsini alikuwa na kete hizo tumboni mwake zikiwa na uzito wa kilo moja na nusu.

Jeshi la Polisi visiwani humo limewataka watu wote wanaojihusisha na biashara hiyo haramu kuachana nayo kwani Jeshi la Polisi liko makini.

error: Content is protected !!