Wafukua kaburi la mwenye ualbino na kuondoka na viungo

HomeUncategorized

Wafukua kaburi la mwenye ualbino na kuondoka na viungo

Watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Tanga kwa madai kufukua kaburi la kijana mmoja mwenye ualbino na kutoweka na jeneza na mabaki ya mwili wake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Safia Jongo, amesema Polisi inawashikilia watu hao watatu na kuhifadhi majina yao ili kuendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Imeelezwa kwamba, Heri Kijangwa (45), alifariki Julai 4, 2021 na alizikwa Julai 7, 2021 katika kijiji cha Tandwa wilayani Lushoto.

0ctoba 26 mwaka huu, familia ilikuta kaburi limefukuliwa huku jeneza pamoja na mabaki ya mwili wa marehemu vikiwa vimechukuliwa.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la ‘Under the Same Sun’ Peter Ash amesema “Heri alikuwa ni mnufaika wa programu za elimu, tunasikitika sana kwa unyama huu”

Peter Ash amesema shirika lake (Under The Same Sun) lilimsomesha kijana huyo na kabla ya mauti alikuwa anachukua Shahada ya Uzamili ya Afya ya Jamii katika Chuo Kikuu cha Muhimbili, akiwa amemaliza shahada ya kwanza ya Sayansi ya Kimataifa na Teknolojia mwaka 2015.

Heri Kijangwa alifariki kutokana na maradhi ya saratani ya ngozi.

error: Content is protected !!