Alichokiomba mtoto wa Simbachawene kwa hakimu

HomeKitaifa

Alichokiomba mtoto wa Simbachawene kwa hakimu

Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, imemhukumu James Chawene (24), mtoto wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene kulipa faini ya Sh250,000 au kwenda jela miaka 2.6 baada ya kuthibitika kuwa na makosa matatu likiwamo la kuendesha gari akiwa amelewa.

Mtuhumiwa huyo alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Aron Lyamuya na alikiri mashtaka aliyosomewa. Baada ya kukiri makosa Hakima Lyamuya alisema ametiwa hatianai kwa makosa yake.

Hakimu Lyamuya alisema kitendo alichokifanya ni hatrai kwa usalama wa watumiaji wengine wa barabara kwani angeweza kuleta madhara zaidi.

Alipopewa nafasi ya kujitetea ili asipewe adhabu kali, kupitia wakili wake, Alfred Mtawa, mhstakiwa alisema ana mke na mtoto mchanga wanaomtegemea.

“Mheshimiwa hakimu najutia makosa yangu niliyoyafanya hivyo naomba mahakama yako inionee huruma na kunipunguzia adhabu kwa sababu ni kosa langu la kwanza na nimeshayatengeneza magari niliyoyasababishia uhalibifu,” alisema.

Pia, aliomba asifungiwe leseni kwa kuwa yeye ni mfanyabiashara na anatumia gari kila siku hivyo itamuathiri katika shughuli zake.

 

error: Content is protected !!