Alichosema Fatma Karume kwenye Kikosi Kazi

HomeKitaifa

Alichosema Fatma Karume kwenye Kikosi Kazi

Aliyewahi kuwa Rais wa Chama cha wanasheria Tanganyika (TLS) Fatma Karume, ameshauri uwepo wa mfumo wa muungano wa seriklai tatu tofauti na uliopo hivi wa serikali mbili huku akipendekeza kuanza haraka mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya.

Wakili huyo wa kujitegemea ni mtoto wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati akitoa mapendekezo yake mbele ya Kikosi Kazi cha Rais Samia Suluhu Hassan ambacho ni maalumu kwa ajili ya kukusanya maoni kuhusu demokrasia na vyama vya siasa.

“Kutokana na mitazamo hiyo kuna mgongano kati ya wanasiasa na CCM na watu wa UKAWA na maoni ya wananchi wenyewe wanaotaka serikali tatu, CCM wanadhani tukiwa na muundo wa Serikali tatu pengine nchi itapasuka,

“Ni vizuri kuweka mchakato huo badala ya kuendelea kuwiata wahaini wanaoonekana kupinga muungano uliopo na hasa kwa sasa kuna Watanzania wengi ambao inawezekana hawataki muungano wapewe nafasi ya kusikilizwa,” alisema Fatma Karume.

Wakili huyo wa kujitegemea alipendekeza pia yapunguzwe madaraka ya Rais ili kumfanya asiwe kama sultani hasa kwa kumpa majukumu ya kufanya teuzi mbalimbali zikiwemo za majaji na wakuu wa mikoa.

“Rais asiwe na uwezo wa kuchagua Kamanda wa Jeshi la Polisi(IGP) na watendaji wa kudumu, kwani nafasi hizo zinatakiwa zizingatie weledi kwa sababu wanatoa huduma kwa jamii badala ya siasa kama ilivyo sasa,”alisema.

Mwanasheria huyo alisisitiza kwamba ni lazima Katiba Mpya ipatikane ili kumpunguzia Rais hayo madaraka na ili ipatikane katiba lenye kulinda maslahi ya wananchi ni lazima iundwe kamati ya wataalamu wabobevu wa sheria na katiba na si wanasiasa.

error: Content is protected !!