Mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya SEkondari Msimbati, Taufiq Hamisi (15) ambaye aliandika barua ya kuacha shule kutokana na ugumu wa maisha amepata ufadhili wa kuendelea na masomo katika shule ya Sekondari ya Ocean iliyopo Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Meneja wa shule ya Ocean, Juma Nchia alieleza kuwa taasisi mbili za Kalamu Education Foundation (KEF) pamoja na Mar’wa Education Centre inayomiliki shule ya Ocean kwa kushirikiana na wadhamini mbalimbali, wameamua kuwachukua wanafunzi wawili na kuwahamishia katika shule ya Sekondari ya Ocean.
“Taasisi ya elimu ya Kalamu itakuwa ikiwasiliana na wadau mbalimbali wa elimu na kufuatilia maendeleo ya wanafunzi hao kisha kutoa ripoti,”
‘Tunaomba wafadhili wajitokeze kwa wingi kusaidia watoto, elimu ni bure lakini bado watoto wanahitaji vifaa, sare na mahitaji mengine muhimu pia,” alisema Nchia.
Kwa upande wake Taufiq, alishukuru wahisani hao na kusema kuwa sasa ndoto zake za kuwa rubani wa ndege zitatimia.