Aliyejioa ajipa talaka baada ya siku 90 ya ndoa yake

HomeKimataifa

Aliyejioa ajipa talaka baada ya siku 90 ya ndoa yake

Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Cris Galera mwenye umri wa miaka 33 alishika vichwa vya habari baada yakujioa miezi mitatau iliyopita, lakini ameamua kujipa talaka kwa kile kinachoelezwa kwamba amepata mtu wakuwa naye katika mahusiano.

Harusi yake ilifanyika Septemba mwaka huu huku akitaka kurasimisha muungano kati yake na yeye mwenyewe na kusema chanzo cha kuchukua maamuzi hayo ni kuchoshwa kuumizwa na wanaume hivyo ni bora ajioe.

Mwanamitindo huyo wa Instagram, sasa ameomba talaka kwake kwani alikutana na mtu mwingine ambaye anatarajia kufunga naye ndoa.

Takriban siku 90 baadaye, inaonekana kwamba Galera hawezi tena kukaa kwenye ndoa na yeye mwenyewe. Amesema kwamba, kadiri alivyofurahia siku ya harusi na hadithi yake kusambaa, ilikuja na maoni yasiyo ya kirafiki kutoka kwa umma ambao ulikosoa uamuzi wake. Hata hivyo, aliweza kuinua kichwa chake juu kwa kuwapuuza na kuzingatia maisha yake.

error: Content is protected !!