Ugonjwa wa wanawake kuota nywele kifuani na usoni

HomeElimu

Ugonjwa wa wanawake kuota nywele kifuani na usoni

Baadhi ya wanawake wamekua na nywele maeneo ya kifua na usoni. Kitaalamu hii hali huitwa “Hirsutism” ambapo madaktari hufanya uchunguzi juu ya tatizo hilo kwa kupima kiwango chako cha homoni na kufanya Ultrasound ili kuchunguza Ovari na Uterasi.

Zipo sababu kubwa zinazopelekea mwanamke kuota nywele usoni na kifuani nazo ni kama zifuatazo

1. Ugonjwa wa PolystyticsPolystytics ni ugonjwa unaosababisha hitilafu katika Homoni za wanawake. Homoni za mwanamke zinapokua zinaharibiwa, husababisha mabadiliko mbalimbali katika mwili na moja wapoo ni kuota nywele kifuani na usoni. Tofauti na hilo, ugonjwa huu husababisha mwanamke kupata hedhi isiyo ya kawaida na maumivu yta nyonga.Jinsi ya kuepukana na ugonjwa wa PCS ni kupitia lishe bora, kufanya mazoezi ya kila mara na pia kupata matibabu yanayofaa kutoka kwa madaktari bingwa wa afya ya uzazi.

2. Madhara yatokanayo na MadawaDawa zimetengenezwa kwaajili ya kutibu magonjwa ili tupate ahueni ya maradhi, ila baadhi ya dawa husababisha madhara hasi kwa binadamu na moja kati ya madhara ni kuota nywele kwa wanawake. Mfano wa dawa hizo ni glukokotikoidi zinazotumika kutibu uvimbe.

https://clickhabari.com/mambo-4-ya-kuzingatia-kwenye-ufugaji-wa-ndevu/

3. Tatizo la Homoni
Mwanamke anapokua anashida ya homoni inapelekea kuzalisha homoni za kiume zaidi katika mwili, homoni kama “Androgen” husababisha mwanamke kuwa na sifa mbalimbali zinzoendana na mwanaume ikiwemo utoaji wa nywele kifuani nja usoni mfano wa ndevu.

4. Uzito Mkubwa
Wanawake wanapokuwa na uzito mkubwa, miili yao huzalisha homoni nyingi za kiume na hii hupelekea nywele nyingi usoni na mwilini.

Lakini pia sababu zingine kwa nini wanawake wanaweza kuwa na nywele nyingi usoni na sehemu nyingine isivyo kawaida, ni sababu za urithi. Ikiwa ‘hirsutism’ iko katika familia, basi wengine wanaweza kuwa nayo. Pia kuna sehemu kubwa ya wanawake katika jamii fulani wanaweza kuwa na nywele nyingi usoni, mfano wanawake wa Asia ya Kusini, Mediterania na Mashariki ya Kati.

error: Content is protected !!