Mambo 4 ya kuzingatia kwenye ufugaji wa ndevu

HomeElimu

Mambo 4 ya kuzingatia kwenye ufugaji wa ndevu

Ndevu zinaweza kumuongezea mtu muonekano mzuri kama tu anazitunza vyema katika hali nadhifu. Sio kila mtu amebahatika kupata ndevu, wengine ndevu zao huota haraka, wengine huoba kwa kuchelewa na wengine hawana kabisa. Kwa wale wapenzi wa ndevu, zipo hatua kadhaa za kufuata ili kupata nzuri nzuro. Ili sasa kuanza safari yako kufunga ndevu, basi zingatia yafuatayo.

  1. Uvumilivu
    Kutokana na kutofautiana lisha, matumizi ya vipodozi na hata vinasaba, uotaji wa ndefu wa watu hufautiana. Kwa wengine Inaweza kuchukua mwezi au wengine hata mwaka ili ndevu ziweze kuota hivyo basi uvumilivu ni kitu muhimu unachopaswa kuzingatia. Usinyoe kwani haitosaidia kukua ndevu kwa haraka.
  1. Kufanya mazoezi
    Mazoezi si tu kwa ajili ya afya yako bali husaidia uzalishaji wa testosterone ambapo kama itazalishwa kwa wingi basi ndevu zitaota haraka na vizuri.
  1. Lishe
    Kwa wale ambao ndevu zina viraka ama kuna sehemu hazijajaa vizuri na wale wanaotaka kuongeza ujazo wa ndevu, basi sasa ni wakati wa kuhakikisha unazingatia lishe mfano unaweza kula sana vyakula vya protini kama mayai na samaki.
  1. Matunzo
    Jenga na endeleza matumizi ya mafuta ya ndevu kama beard nourishing oil, beard balm, beard conditioner na beard butter. Kila mmiliki wa ndevu anapaswa kuwa na vifaa kam amashine ya kuchongea ndevu (Trimmer), Chanuo na brashi.

Hivyo basi katika safari yako ya ufugaji ndevu jaribu kuzingatia mambo hayo 4.

error: Content is protected !!