Simba yapata pigo la viungo

HomeMichezo

Simba yapata pigo la viungo

Timu ya soka ya Simba ya jijini Dar es Salaam imepata pigo baada ya viungo wake wawili, Mzamiru Yassin na Sadio Kanoute kuripotiwa kwamba wataukosa mchezo ujao dhidi ya Namungo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotoka ndani ya Simba, Mzamiru na Kanoute watakaa nje katika mchezo ujao kutokana kuendelea kuuguza majeraha waliyoyapata katika mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union.

Daktari wa Simba, Yassin Gembe amesema wachezaji hao hawakupata majeraha makubwa lakini wataukosa mchezo wa kesho ili kuwakinga wasiumie zaidi na kuwapa nafasi ya kupona vizuri.

Hali hiyo inaweza kuwafanya Simba wamuanzishe Jonas Mkude ambaye aliingia kipindi cha pili katika mchezo uliopita baada ya kukalia benchi kwa muda mrefu.

Simba itashuka dimbani kesho katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuumana na Namungo katika mchezo wa Ligi Kuu huku mashabiki wa timu hiyo wakitarajia matokeo chanya kufuatia kutoridhishwa na mwenendo wa mabingwa hao watetezi.

error: Content is protected !!