Njia za kukuza nywele na kuzuia kukatika

HomeElimu

Njia za kukuza nywele na kuzuia kukatika

Matunzo ya nywele yanahitaji kuwa na moyo na uthabiti katika kuhakikisha zipo kwenye hali nzuri mara zote lakini pia kutafuta muda wa kuzifanyia matunzo japo mara moja kwa wiki.

Watu kutoka tamaduni mbalimbali duniani wamekuwa wakija na njia tofauti tofauti za kukuza nywele ambazo huongeza utanashati na urembo kwa wadada na zipo mbinu ambazo zimeonekana kuwa na matokeo mazuri zaidi.

Maji

Haya ni maji ya kawaida kabisa ya bombani. Maji husaidia sana katika kuongeza unyevu kwenye nywele, na nywele huhitaji unyevu ili kuzuia kukatika. hata kama umesuka jitahidi kupulizia nywele zako maji walau mara moja kila siku

Maji ya mchele

Maji ya mchele yamekuwa yakitumiwa kukuza nywele hasa kwa Wayao ambao wamejizolea umaarufu kwa kuwa na nywele ndefu. Osha mchele wako kikombe kimoja kisha uloweke kwenye maji vikombe viwili kwa siku moja hadi mbili hadi maji yachachuke. Unaweza kuongeza mafuta ya maji na ganda la machungwa au limao kukata harufu mbaya na kuongeza mafuta kwenye nywele. Weka maji hayo kwenye chupa unayoweza kupulizia na upulizie kwenye nywele kwa wiki mara tatu hadi nne. Pia unaweza kusuuzia nywele baada ya steaming. Madini yaliyopo kwenye maji ya mchele yaliyochachuka husaidia kujaza nywele na kuzifanya ziimarike.

Maji ya uwatu

Uwatu ama fenugreek husaidia pia kupunguza tumbo lakini inapokuja kwenye nywele kama ilivyo kwa mchele loweka mbegu za fenugreek kisha yale maji pulizia kwenye nywele zako  kama ambavyo ungefanya kwa maji ya mchele

Tumia aloe vera

Pasua aloe vera katikati na baada ya kuosha nywele zako unaweka kuchukua ute wa aloe vera ukachanganya na mafuta ya maji unayopenda kisha ukapakaza kwenye nywele na kuziacha kwa dakika 20 hadi 30 na kuzisuuza kisha uendelee na kuzikausha na kusuka.

Mafuta ya moto

Simaanishi yaliyochemka ila ‘hot oil treatment’ hufanywa kwa kuchemsha maji ya moto na kuchukua chupa yenye mafuta ya nywele kimiminika na kukiweka mwenye maji ya moto hadi yapate joto la kutosha kisha paka kwenye ngozi ya kichwa na kumassage taratibu. Hii husaidia kufungua matundu ya nywele na kuzipa nywele nafasi ya kukua kwa urahisi.

Kata ncha

Wanasema nywele za mwafrika hazikatwi ncha ila si kweli. Nywele ikichoka hutengeneza ncha ambayo hufanya nywele zidumae na kuanza kukatika lakini kama utakata ncha walau mara mbili kwa mwaka utakuwa umesaidia nywele zako badala ya kukatika zenyewe kwa kukosa afya bali zitaota na kufikia urefu unaoutaka.

error: Content is protected !!