Kajala achorewa tattoo

HomeBurudani

Kajala achorewa tattoo

Shabiki mmoja wa mwanamuziki Harmonize ameamua kuingilia kati jitihada za mwanamuziki huyo za kurudiana na ‘ex’ wake Kajala Masanja.

Shabiki huyo amejichora tattoo ya barua katika jitihada za kumsaidia Harmonize kuomba msamaha kwa Kajala.

Katika tattoo hiyo shabiki huyo ameandika  ” Dada yangu Kajala Masanja, wewe ndio furaha ya moyo wake. Uwepo wako kwake ni wa thamani sana katika maisha yake. Naomba umsamehe Harmo, mpe nafasi nyingine moyoni mwako.”

Na kumalizia kwa kumkaribisha na kumwambia kuwa kama mashabiki bado wanampenda.

Kwa muda sasa Harmonize amekuwa akimuomba Kajala warudiane bila mafanikio baada ya kijana huyo kutaka kula jongoo na mti wake.

Amekuwa akiandika kumwomba msamaha mtandaoni, kwenye jukwaa la Tuzo za Muziki Tanzania, pia alinunua gari aina ya Range Rover kwenye jitihada hizo ambazo zimegonga mwamba.

 

error: Content is protected !!