Meya wa zamani wa Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Juma Raibu aliyevuliwa wadhifa huo baada ya kupigiwa kura za siri na madiwani za kukataliwa amejitokeza tena kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania nafasi hiyo.
Juma Raibu aling’olewa katika wadhifa huo Aprili 11 mwaka huu, baada ya madiwani kupiga kura za siri na kati ya kura 28 zilizopigwa, 18 zilikataa asiendelee na wadhifa huo huku 10 zikimtetea abaki katika nafasi hiyo aliyodumu nayo tangu ulipokamilika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Moshi mjini, Raibu amesema ameamua kurudi kuwania nafasi hiyo kwa kuwa toka ameondolewa kwenye nafasi hiyo, baada ya kuona Moshi imepoa na kuwepo kwa vurugu nyingi.