Aliyosema Rais Samia kuhusu utendaji kazi wa marehemu Ole Nasha

HomeKitaifa

Aliyosema Rais Samia kuhusu utendaji kazi wa marehemu Ole Nasha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameeleza kupokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha aliyekuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, William Tate Ole Nasha.

Ole Nasha ambaye pia alikuwa Mbunge wa Ngorongor kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) amefariki Dunia Septemba 27, 2021 usiku jijini Dodoma.

Rais Samia amemuelezea Marehemu Ole Nasha kuwa alikuwa mchapakazi na hodari katika sekta aliyokuwa, na mtumishi mwaminifu kwa Serikali na pia ametoa mchango mkubwa katika ujenzi wa Taifa.

Aidha, ametoa pole kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, wabunge, familia ya marehemu na wananchi wa Ngorongoro.

error: Content is protected !!