Mwanamuziki R. Kelly akutwa na hatia

HomeKimataifa

Mwanamuziki R. Kelly akutwa na hatia

Msanii gwiji wa miondoko ya RnB, Robert Kelly, maarufu R. Kelly amekutwa na hatia ya makosa ya ukatishaji fedha, kujipatia fedha kwa nguvu pamoja na kusafirisha binadamu. R. Kelly amekutwa na hatia hiyo baada ya kesi yake kusikilizwa kwa wiki sita mfululizo.

Mwanamuziki hayo alipata shutuma hizo tangu miongo miwili iliyopita, lakini kesi dhidi yake haikufunguliwa kutokana na kukosekana kwa ushahidi, hadi pale wahanga kadhaa walipojitokeze kupitia vipindi vya mahojiano ya runinga na kutoa tuhuma dhidi yake.

Wahanga tisa walifungua mashtaka dhidi yake, wakiwa wanawake saba na wanaume wawili kwa makosa ya unyanyasaji wa kijinsia na ubakaji.

Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 54 hukumu yake inatarajiwa kutolewa Mei 4, 2022, kwa sasa ataendelea kuwa kizuizini kwa usalama wake.

error: Content is protected !!