Amteka nyara mtoto wake, amuua kisha kujinyoga.

HomeKimataifa

Amteka nyara mtoto wake, amuua kisha kujinyoga.

Mwanaume mmoja jijini Nairobi aliyetambulika kwa jina la Victor Aiyeko anasemekana kumteka nyara mtoto wake mwenye umri wa miaka 3, kumuua na kisha kujinyonga mwenyewe  baada ya kuingia kinyemelea nyumbani kwa mke wake wa zamani alipokuwa ametoka kwenda kazini.

Baada ya mama wa mtoto huyo ,Nancy Adhiambo na mumewe Christopher Okeyo kurudi nyumbani waliambiwa na majirani kwamba mume wake wa zamani alionekana akiondoka na mtoto wake kwenye pikipiki na ndipo wawili hao walikimbia hadi nyumbani kwa Ayieko na kukuta maiti ya mtoto huyo kitandani huku Ayieko akiwa amejinyonga kwajininginiza juu kwenye kebo ya umeme.

Maafisa wa Polisi wamesema kwamba marehemu Ayieko aliacha ujumbe uliomtaka mke wake wa zamani atoe taarifa kwa ndugu zake kuhusu kifo hicho kwa kutumia noti ya Ksh.500 aliyoiacha.

Aidha Polisi wamewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawaacha watoto kwenye mikono salama pindi waendapo kazini.

“Kutokana na ongezeko la visa vya kupotea kwa watoto katika mashamba ya jiji, wazazi na walezi wanahimizwa kuhakikisha usalama na usalama wa watoto wao, kwa kuwaacha mikononi mwa watu wazima wanaowajibika kila wanapokuwa mbali,” DCI ilisema.

error: Content is protected !!