‘In my Maserati’ yamlambisha dili nono Olakira

HomeBurudani

‘In my Maserati’ yamlambisha dili nono Olakira

Mwimbaji anayekuja kwa kasi kutoka nchini Nigeria, Olakira, ameanza mwaka kwa njia nzuri kwa kusaini mkataba  na kampuni ya magari ya kifahari, Maserati na hii ni kwa sababu ya  wimbo wake mkali, ‘In My Maserati’, ambao uliongoza chati kwa wiki nyingi zaidi Nigeria na duniania kwa ujumla.

Taarifa hizo zimejulikana baada ya msanii huyo kuweka video kwenye ukurasa wake wa Instagram ikimuonesha mwenye furaha baada ya kuambiwa habari hizo njema huku moja wapo ya makubaliano ya mkataba huo ni kwamba Olakira anaweza kupata na kutumia magari ya kampuni hiyo nchi yoyote atakayotemba.

Kabla yakuanza kufanya kazi zake mwenyewe, Olakira alianza kwa kucheza ala za muziki kanisani na kwenye sherehe mbalimbali huku akilipwa, lakini baadae alianza rasmi zake zake za uimbaji binafsi na kuwa mtayarishaji wa nyimbo.

error: Content is protected !!