Aponzwa na biashara ya vidole

HomeKimataifa

Aponzwa na biashara ya vidole

Mahakama nchini Zimbabwe imemfungulia mashtaka mtu mmoja kwa kufanya mzaha kuwa alikuwa sehemu ya kundi la watu wanaonunua vidole vya miguu vya binadamu kwa hadi dola za Marekani 78,000.

Hivi karibuni madai kwamba Wazimbabwe wameamua kuuza vidole vyao vya miguu yalienea kwenye mitandao ya kijamii ambapo afisa wa ngazi ya juu wa Serikali alikanusha utani huo akisema hilo ni jaribio la kuharibu taswira ya nchi hiyo.

David Kaseke, mfanyabiashara wa simu za mkononi patika Jimbo la Harare mwenye umri wa miaka 40 alionekana kwenye video akisema alikuwa sehemu ya harambee ya kununua vidole vya miguu vya binadamu kwa kati ya dola za Marekani 26,000 na 78,000 ambapo alifikishwa mbele ya Hakimu wa Harare Meenal Narotam na kushtakiwa kwa kosa la jinai.

Kaseke alidai kidole hicho cha mguu mdogo kitagharimu kati ya dola 25,000 na 30,000 huku kidole gumba cha mguu huo kikigharimu dola 75,000.

 

error: Content is protected !!