Askari aliyefukuzwa kazi akiwa hajitambui (coma), azinduka baada ya miezi 9

HomeKimataifa

Askari aliyefukuzwa kazi akiwa hajitambui (coma), azinduka baada ya miezi 9

Afisa wa jeshi la Polisi nchini Kenya ambaye alitoweka na hakujulikana alipo kwa muda wa miezi tisa, kwa sababu hakuna aliyekuwa anajua kama amelazwa hospitali, ametambulika alipo.

Reuben Kimutai Lel ilitangazwa kwamba hajulikani alipo na mamlaka zikasitisha mshahara wake baada ya kumtafuta kwa muda na wasijue alipo. Baada ya harakati za kumpata kugonga mwamba mamlaka ilitoa hati ya kukamatwa, lakini baadae kesi ilifutwa baada ya polisi kushindwa kumpata.

Imebainika kwamba kwa muda wote (Desemba 2020 – Septemba 2021) huo alikuwa hospitali hajitambui, hadi juma lililopita alipopata fahamu. Hata hivyo, licha ya kuwa kumbukumbu zake kamili hazijarejea ameweza kujitambulisha kwa jina na kwamba alikuwa polisi, hivyo mchakato wa kuwapata nduguze ukaanza.

Imefahamika kuwa alipata ajali ya barabarani jijini Nairobi na kupelekewa hospitali Desemba 21, lakini hakuwa na nyaraka yoyote ya kumtambulisha.

Imedaiwa kuwa atarejeshwa kwenye mfumo wa malipo wa polisi.

error: Content is protected !!