Kauli ya Lowassa kuhusu hotuba ya Rais Samia UN

HomeKitaifa

Kauli ya Lowassa kuhusu hotuba ya Rais Samia UN

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Ngoyai Lowassa, ameandika waraka mfupi ambao pamoja na mabo mengine, umepongeza hotuba aliyoitoa Rais Samia jana kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Waraka huo uliosainiwa na Lowassa mwenyewe unasomeka hivi :

“Kwanza nianze kwa kumpongeza na kumshukuru Rais wetu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuifanya vyema kazi ya kujenga nchi na kisha kuendeleza safari ya kujenga uchumi imara.

Kupitia hotuba yake katika Baraza Kuu la Umoja wa mataifa, New York Marekani jana Alhamisi, Mama Samia amelirejesha tena taifa letu katika ramani ya dunia.

Katika kipindi kifupi alichokuwa madarakani, Rais Samia amefanikiwa kuanza kujenga imani ya sekta binafsi katika kushiriki kwenye ujenzi wa uchumi.

Safari ambayo hatuna budi sote kumuunga mkono na kumsaidia ili aliwezeshe taifa kuwa imara zaidi kiuchumi na kuiweka nchi katika utawala wa sheria.

Rais Samia amethibitisha pasi na shaka kwamba Tanzania imepata nyota ya jaha kwa kuwa na kiongozi mkuu mwanamke hodari na shupavu ambaye leo hii tuna kila sababu ya kujivunia na kumuunga mkono”

error: Content is protected !!